Sunday, 12 February 2017

Mwimbaji wa bongofleva Barnaba ambaye ni miongoni mwa waliotoka mbali wakifahamiana na Diamond Platnumz ameyaandika haya kwenye Instagram page yake leo baada ya kuiweka hii picha ya Diamond akiwa na familia yake.
Ukweli nisiwe muongo kutoka moyoni hii picha inaongea mengi sana nimetazama machozi yamenitoka kabisa kwa furahaa sana, umoja ni nguvu kabisa mkishikana kwa kila matatizo na mkapambana kila kitu kinakua sawa”
Matatizo ni mengi lakini mwanangu Rafiki Yangu @diamondplatnumz nakupongeza sana kwa kusimama na Familya yako kwa kila mitihani na mbali na mambo Yote ya binadamu na maneno masimango Kash kash za Hapa na pale
Picha yenyewe iliyomtoa Barnaba machozi ya furaha
unaonesha Upendo wa wazi na ni wachache wenye kukubali kubeba majukumu na ukubwa wa maisha ni kuyafata majukumu sio kuyakimbia Mungu akubariki Asante sana kwa mualiko pia nashukuru sana tuko pamoja mpaka mwisho mimi nakuombea na Mungu Akusimamie Amina uku mama uku mkwe uku ubavu wako kati Marafiki wako wa milelee watoto wako aisee

No comments:

Post a Comment