Sunday, 12 February 2017

MANENO YA T.I.D BAADA YA KUKUTANA NA MHESHIMIWA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM PAUL MAKONDA


Jana February 11 2017 Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda alimualika nyumbani kwake Masaki mwimbaji maarufu wa Bongofleva T.I.D ambaye siku 3 zilizopita aliachiwa kwa dhamana baada ya kulazwa Polisi kwa tuhuma za utumiaji wa dawa za kulevya.
Leo Paul Makonda alipomuita T.I.D nyumbani kwake walizungumza mambo mengi  na baadae mkuu huyo wa mkoa akaandika “Mungu wetu hajalala na siku zote anampenda amtafutae, karibu tena nyumbani T I D”
Sasa na T.I.D nae ameamua kuandika yafuatayo baada ya kukutana na Paul Makonda ambapo aliyaambatanisha maneno hayo na picha waliyokaa pamoja >>> “Muziki bila Madawa ya kulevya inawezekana…This is the turning Point kwangu mimi na kizazi cha mziki huu wa kizazi kipya”
Akamalizia kwa kuandika “Nikiwa na Mh. Makonda leo tukijadili jinsi gani ya kuokoa Vipaji na Sanaa kwa ujumla, Mungu ibariki Bongo Fleva,Mungu Ibariki Tanzania

No comments:

Post a Comment